Waziri Mkuu Wa Ethiopia : Jeshi La Ethiopia Limechukua Udhibiti Wa Mekele

 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema majeshi ya nchi hiyo yamechukua udhibiti wa mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle. 

Abiy ametangaza kuwa serikali ya shirikisho sasa imechukua udhibiti kamili wa mji huo ikiwemo uwanja wa ndege, taasisi za umma, ofisi za utawala wa jimbo hilo na maeneo mengine muhimu.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Twitter siku ya Jumamosi, Abiy ametangaza pia kuwa wamemaliza operesheni yao ya kijeshi katika jimbo hilo.

Abiy ameongeza pia kuwa maelfu ya wanajeshi ambao walikamatwa na wapiganaji wa chama tawala katika jimbo hilo ‘Tigray People's Liberation Front'- TPLF, yaani Chama cha Ukombozi wa Watigray pia wameachiliwa huru. 

Chama cha TPLF kimekuwa madarakani katika jimbo hilo la kaskazini mwa Ethiopia.


EmoticonEmoticon