Rais wa
Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba wanasayansi nchini humo wamepiga hatua
kubwa sana katika kupata tiba dhidi ya Corona.
Katika hotuba kwa taifa jana jumapili, Museveni amesema
kwamba wanasayansi nchini humo wamefanyia majaribio tiba hiyo ambayo hakutoa
maelezo zaidi, akiongezea kwamba kwa sasa, madaktari wanatumia mchanganyiko wa
vitu maalum ambavyo vinaongeza kinga mwilini dhidi ya virusi vya Corona.
“wanasayansi wetu wameniambia habari njema kwamba wameunda
dawa saba tofauti. Sita kati ya hizo zinafanyiwa majaribio na moja inaongeza
kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona.” Amesema Museveni katika hotuba
iliyopeperushwa na runinga zote za habari nchini Uganda, akiongezea kwamba
“dawa za kwanza tatu zinauwa virusi hivyo na kuzuia uharibifu mwilni.”
Museveni amesema kwamba dawa hiyo imefanyiwa “majaribio kwa
wagonjwa kadhaa wa Corona na kupona na itaanza kutumika vikamilifu kwa watu wote
Desemba tarehe 15 mwaka huu.”
Ameendela kusema kwamba “katika mda wa siku 40, dawa hiyo
itakuwa imetibu watu wengi na kuweka Imani kati yaw engine kwamba inaweza
kutibu Corona na virusi vingine.”
Museveni ameongezea kusema kwamba “wanasayansi wa Uganda wamezindua
vipimo vya Corona kwa kuumia sampuli ya mate na kutoa matokeo ndani yam da wa
dakika 30.”
Jumla ya watu 210 wamefariki kutokana virusi vya Corona
nchini Uganda.
Kampuni kadhaa nchini Marekani na ulaya zimetangaza kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona.
Credit: Voa
EmoticonEmoticon