Aina Mpya Ya Kirusi Cha Corona Yaripotiwa Marekani

 

Aina mpya ya kirusi cha corona kinachoaminka kusambaa kwa kasi, imeripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani na Amerika ya Kusini wakati rais mteule wa Marekani Joe Biden akiapa kuzidisha juhudi za utoaji wa chanjo. 

Aina hiyo mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, sasa kimeripotiwa kuingia Marekani katika mji wa Colorado. Kirusi hicho kimegundulika kwa kijana wa miaka 20 ambaye hana historia ya kusafri. 

Taarifa za vyombo vya habari za ndani zinasema kuna uwezekano wa kisa kingine cha kirusi hicho. Wataalamu wanaamini kwamba aina hiyo mpya inaweza kuenea kwa kasi na itakuwa chanzo cha ongezeko la maambukizi Uingereza. Aina hiyo mpya ya kirusi kinachujulikana kama B.1.1.7 tayari pia imeripotiwa Canada, Italia, India na Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Chile nayo imeripoti aina hiyo mpya na kulifanya kuwa taifa la kwanza Amerika ya Kusini kubaini maambukizi yake.Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameonya kwamba hali mbaya ya Covid-19 inaweza isiwe rahisi hadi kufikia mwezi Machi. 

Aidha Biden ameongeza kuwa changamoto iliyopo ni kampeni kubwa ya utoaji chanjo huko akiukosoa mpango wa mtangulizi wake Donald Trump katika usambazaji chanjo.

"Lakini kama nilivyohofia na kuonya kwa muda mrefu, juhudi za kusambaza na kutoa chanjo haziendelei kama inavyostahili. Wiki chache zilizopita, utawala wa Trump ulipendekeza kwamba Wamarekani milioni 20 wangeweza kupewa chanjo kufikia mwishoni mwa Desemba. Ikiwa hali itaendelea kama ilivyo sasa, itachukua miaka, sio miezi, kuwapatia chanjo raia wa Marekani" alisema Biden.


EmoticonEmoticon