Mwanaume
mmoja nchini Kenya aliyedhaniwa amefariki dunia na kupelekwa chumba cha
kuhifadhia maiti na "kupata tena fahamu" wiki jana, sasa amefariki
kweli, kulingana na vyombo vya habari vya eneo.
Wiki iliyopita, inasemekana kuwa
mhudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti alikuwa anatayarisha mwili wake kuuweka
kwenye chumba maalum kwa ajili ya wafu, kabla ya mwanaume huyo kupata fahamu
ghafla na kuanza kupiga kelele.
Peter Kigen, 32, ambaye alikuwa
ameugua kwa muda mrefu, alipekwa hospitali kupata matibabu na baadaye,
akaruhusiwa kwenda nyumbani.
Akizungumza na gazeti la Kenya la
Daily Nation, Alhamisi iliyopita, alisema kwamba ni mwenye furaha kuwa hai.
"Hii ni kazi ya Mungu," ameliambia gazeti hilo.
Tukio hilo lilisabisha wengi kutoa
maoni yao katika mitandao ya kijamii, na pia likajadiliwa katika bunge la
kaunti ya Kericho.
Bunge hilo liliunda timu kuchunguza
kile hasa kilichotokea taarifa ambayo iliwaondolea wahudumu wa afya lawama.
Alhamisi, msemaji wa familia
alithibitisha kifo cha kweli cha mwanaume huyo kupitia gazeti za Kenya la
Standard.
"Kigen alitangazwa kufariki dunia baada ya kufika hospitali ya kaunti ya Kericho alikopelekwa kutoka hospitali ya Kapkatet kwa matibabu zaidi," Hezbon Tonui amesema.
EmoticonEmoticon