Angela Merkel Asema Misaada Kwa Wafanyabiashara Haiwezi Kuendelea Milele

 

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hapo jana kwamba misaada ya serikali kwa wafanyabiashara inayotolewa katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya corona haiwezi kuendelea milele. 

Merkel ameyasema hayo kabla ya mkutano wa kujadili bajeti ya serikali ya mwaka ujao 2021. Siku ya Jumanne Bunge la Ujerumani - Bundestag- linatarajiwa kujadili bajeti ya serikali iliyopendekezwa kwa mwaka ujao, ambayo theluthi moja itafadhiliwa kwa mkopo. 

Serikali ya shirikisho ya Ujerumani inapanga kukopa euro bilioni 180 za ziada kwa mwkaa ujao, huku Merkel akijaribu kutetea ongezeko hilo la deni la serikali. 

Merkel amesema hasara itakuwa kubwa zaidi, kifedha na kijamii, ikiwa biashara zitaporomoka na mamilioni ya ajira kupotea. Ameongeza kwamba mwakani serikali itatumia pia akiba ya fedha zilizoweza kuhifadhiwa katika miaka ya hivi karibuni.


EmoticonEmoticon