Atozwa Faini Ya Milioni 8 Kwa Kutoka Nje Ya Chumba Kwa Sekunde 8

 

Serikali ya Taiwan imemtoza faini ya USD 3500 (zaidi ya Tsh. milioni 8) Mwanaume mmoja kutoka Ufilipino kwa kosa la kuvunja masharti ya corona kwa kutoka nje ya chumba chake cha Hoteli kwa sekunde 8 tu kama alivyoonekana kwenye camera za usalama.

Mwanaume huyo ambae ni Mgeni kutoka Philippines alikua sehemu ya Watu walioweka karantini Hotelini huko Kaohsiung Taiwan ambako Hotel 56 zinatumika karantini zikiwa na vyumba 3000 jumla.

Taiwan yenye Watu milioni 23 ni miongoni mwa sehemu zilizofanikiwa kuidhibiti sana corona ambapo toka corona ianze imepata vifo 7 peke yake na Wagonjwa 716.


EmoticonEmoticon