Rais mteule
wa Marekani Joe Biden amefanya mkutano kwa njia ya video na wafanyabiashara
wadogo wadogo na wafanyakazi ambao wameathiriwa pakubwa kiuchumi kutokana na
janga la virusi vya Corona.
Biden amesimamia mkutano
huo kutoka nyumbani kwake - Wilmington, Delaware, ambapo anafanyia shughuli
zake za kujitayarisha kuingia madarakani baada ya kuapishwa Januari 20.
Vile vile, anaendele
kupokea taarifa za kila siku kutoka kwa maafisa wa ujasusi wa Marekani kuhusu
usalama nchini Marekani na sehemu nyingine zinazoangaziwa sana duniani.
Biden anakabiliwa na
changamoto kubwa ya uchumi ambao umedorora kutokana na janga la virusi vya
Corona atakapoingia madarakani hata wakati kuna matarajio ya kuanza kutolewa
chanjo dhidi ya virusi hivyo baadaye mwezi huu.
Kulingana na chuo kikuu
cha Johns Hopkins, maelfu ya watu wanaripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona
nchini Marekani kila siku, watu 272,000 wamefariki.
Marekani inaongoza kwa idadi ya vifo na maambukizi kutokana na Corona kote duniani.
EmoticonEmoticon