Bobi Wine Aahirisha Kampeni Za Urais

 

Mgombea wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika zaidi kama Bobi Wine, ameahirisha kampeni zake, kufuatia kujeruhiwa kwa maafisa wake wa kampeni na kuharibiwa kwa gari lake.

Kiongozi huyo wa upinzani anasema risasi zilifyatuliwa kwenye gari lake na kutoboa mataili ya gari lake na kumfanya asiweze kusafiri tena.

Video zilizosambazwa na timu yake ya kampeni kwenye mitando ya kijamii zinaonesha kitu ambacho hakikutambuliwa kikilipika umbali wa mita kadhaa kutoka mahali alipokuwa.

Awali katika eneo la Kayunga, mashariki mwa Kampala, gesi za kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wake.

Maafisa wanne wa kampeni yake walijeruhiwa. Mmoja wao, aliyetambuliwa kama producer Dan Magic alipigwa usoni kwake. Mmoja wa polisi wanaowalinda wagombea wa urais waliotolewa na Tume ya Uchaguzi pia alijeruhiwa.


EmoticonEmoticon