Kundi la
wapiganaji la Boko Haram limeaua watu 10 wakiwemo maafisa wanne wa usalama
baada ya kushambulia vijiji vitatu kaskazini mwa Nigeria.
Wapiganaji
hao wamevamia vijiji vya Shafa, Azare na Tashan Alade katika jimbo la Borno, na
kuchoma moto nyumba kadhaa zikiwemo ofisi za serikali kabla ya kufyatua risasi
kiholela dhidi ya wakaazi wa vijiji hivyo.
Wapiganaji
hao walishambulia Kijiji baada ya kingine.
Katika Kijiji
cha Azare, walichoma moto kituo cha polisi na kuua maafisa wawili wa polisi,
mwanajeshi na afisa wa ujasusi.
Wakaazi wa
vijiji hivyo walitorokea msituni kufuatia mashambulizi hayo.
Kundi la Boko
Haram limeongeza mshambulizi dhidi ya raia katika siku za hivi karibuni.
Kundi hilo
limedai kuhusika na shambulizi lililoua watu 11 na kuteka nyara watu mkesha wa
krisimasi.
Kulingana na umoja wa mataifa, kundi la Boko Haram limeua zaidi ya watu 36,000 kaskazini mashariki mwa Uganda na kusababisha karibu watu milioni 2 kutoroka makwao tangu mwaka 2009.
EmoticonEmoticon