Bomu Lililotegwa Kwenye Gari Limewaua Watu Tisa Nchini Afghanistan

 

Mlipuko wa bomu lililotegwa garini mapema leo, umeuwa watu tisa na kujeruhi wengine takirabini 20 mjini kabul, Afghanistan. 

Waziri wa Mambo ya Ndani wa taifa hilo, Masoud Andarabi amewaambia waandishi wa habari kwamba, mbunge Khan Mohammad Wardak ni miongoni mwa waliojeruhiwa. 

Pamoja na kusema kwamba mbunge huyo yupo katika hali nzuri lakini idadi ya vifo inaweza kuongezeka. Shambulizi hilo lilitokea wakati msafara wa mbunge huyo ukipita katika eneo la makutano ya barabara ya Kabul, katika kitongoji cha Khoshal Khan. 

Hadi sasa hakuna yeyote aliedai kuhusika na mripuko huo. Katika taarifa yake ya kulaani shambulio hilo ambayo inaonekana haikulenga moja kwa moja kulishutumu kundi la Taliban, Rais Ashraf Ghani amesema kundi hilo linapaswa kuacha vurugu dhidi ya raia na likubali kusitisha mapigano ili kuwezesha mchakato wa amani unaoendelea sasa.EmoticonEmoticon