Chanjo Ya Tatu Ya COVID-19 Yapata Mafanikio

 

Chanjo dhidi ya virusi vya corona inayotengenezwa na kampuni ya dawa nchini Uingereza ya AstraZeneca na chuo kikuu cha Oxford imepata mafanikio makubwa katika hatua ya majaribio na sasa iko tayari kuanza kutumika. 

Hayo ni kulingana na mkuu wa kampuni ya AstraZeneca katika mahojiano na gazeti la Sunday Times ambaye amesema chanjo hiyo inaweza kutoa kinga kwa asilimia 100 dhidi ya COVID-19 baada ya mtu kupatiwa dozi mbili. 

Chanjo hiyo ambayo sasa inafanyiwa tathmini na taasisi ya udhibiti wa dawa nchini Uingereza ina ubora sawa na zile ya kampuni za Pfizer-BioNTech na Moderna ambazo tayari zimeanza kutumika. 

Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Telegraph chanjo ya AstraZeneca inaweza kupatiwa ithibati kesho Jumatatu na tayari serikali ya Uingereza imeagiza dozi milioni 100 zinakazotolewa kwa mamilioni ya watu nchini humo.


EmoticonEmoticon