China Kuipiku Marekani Kwa Uchumi Mkubwa Duniani Ifikapo 2028 - CEBR

 

Ripoti iliyochapishwa leo na Kituo cha Utafiti wa Uchumi na Biashara duniani, CEBR, inaonesha kwamba huenda China ikaipiku Marekani na kuwa taifa la kwanza kwa uchumi mkubwa duniani ifikapo mwaka 2028, miaka mitano kabla ya muda ambao ulikisiwa awali. 

Kwa mujibu wa kituo hicho, hilo limechangiwa pakubwa na jinsi mataifa hayo mawili yanavyochukuwa hatua za kuzirejesha chumi zao kwenye hali ya kawaida kufuatia janga la virusi vya corona. 

Ripoti hiyo ya kila mwaka ya CEBR inasema kuwa China imefanikiwa zaidi kwenye kukabiliana na athari za COVID-19 kutokana na hatua zake za awali za kufunga shughuli zote. 

Makisio yanaonesha kuwa ukuwaji wa uchumi wa China ni asilimia 5.7 baina ya mwaka 2021 hadi 2025 kabla ya kushuka kwa asilimia 4.5 baina ya mwaka 2026 hadi 2030. 

Marekani kwa upande wake, itashuka kwa asilimia 1.9 baina ya mwaka 2022 hadi 2024 na kisha asilimia 1.6. Japan itaendelea kushikilia nafasi ya tatu kwenye uchumi duniani.


EmoticonEmoticon