CORONA : Karantini Yaanza Ujerumani

 

Ujerumani Jumatano hii imeanza zoezi la kuiweka nchi nzima katika hali ya kufunga shughuli nyingi za kila siku hadi tarehe 10 mwezi ujao kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona. 

Watu wengine 952 wamekufa leo kutokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani. Taarifa hiyo imetolewa na taasisi ya Robert Koch ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza baada ya maambukizi kuongezeka katika muda wa saa 24 zilizopita.

Taasisi hiyo imesema watu 27,728 wameambukizwa na hivyo kufanya idadi ya maambukizi kufikia takriban watu alfu 30 kwa siku tangu Ijumaa iliyopita. 

Hadi kufikia leo wagonjwa wamelazwa kwa asilimia 83 ya vitanda kwenye wodi za kuwahudumia wagonjwa mahututi.


EmoticonEmoticon