James
Hamblin ni daktari wa Marekani ambaye amekaa bila kuoga tangu mwaka 2015
akifanya utafiti wa kuona kama kuna madhara ya mtu kutooga mara kwa mara.
Amegundua
hakuna madhara, harufu hutokana na bakteria kula mafuta yanayotolewa na mwili
hivyo mtu akiacha kuoga kwa muda mrefu mwili unaacha kutoa mafuta, hivyo
anakuwa hatoi harufu.
Anasema,
mwanadamu hutumia wastani wa miaka miwili kuoga, muda ambao anaweza kuutumia
kukuza Uchumi. Hata hivyo anasisitiza kunawa mikono na sabuni.
Hamblin ana umri wa miaka 37, na ni mtaalamu aliyesomea katika Chuo Kikuu cha Yale, Kitengo cha Huduma ya Afya ya Umma na ni Daktari Bingwa wa Tiba ya Kuzuia Magonjwa.
EmoticonEmoticon