Wadukuzi wa
Iran "huenda walihusika" katika uendeshaji wa tovuti kadhaa na
akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zilikuwa zikiwatumia ujumbe wa vitisho
maafisa wa ngazi ya juu waliyopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka
2020, mashirika mawili ya usalama nchi Marekani yametangaza.
Katika taarifa ya pamoja iliyochapishwa Disemba 23, Shirika
la upelelezi la Marekani FBI na Shirika la usalama wa mtandao na na miundo
mbinu ya usalama (Cisa) zilisema zina taarifa ''za kuaminika'' zinazoashiria
kwamba Iran ilikuwa ikiendesha mpango huo.
Oparesheni hiyo "inaashiria nia ya Iran ya kusababisha
mgawanyiko na kutokuaminiana nchini Marekani na kudhoofisha imani ya umma
katika mchakato wa uchaguzi wa Marekani ", iliongeza.
Tovuti na akaunti ya mitandao ya kijamii zilizo na majina,"Maadui wa Watu" na "Maadui wa Nchi", zilibuniwa mapema mwezi Desemba na kujumuisha majina, picha na maelezo kuhusu mahali wanakoishi maafisa 38 wa serikali kuu na majimbo ya Marekani, pamoja na watu binafsi - ambayo huuza programu ya elektroniki ya kupiga kura na vifaa.
EmoticonEmoticon