Habari Tano Kubwa Za Soka Alhamisi Disemba 17

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi December 17, 2020

1. Juventus wameanza kufanya mazungumzo na wakala wa Paul Pogba, 27, Mino Raiola wakijiandaa kumsajili tena kiungo huyo wa kati wa Manchester.

2. Liverpool wanamnya kiungo wa kati wa Lille na Portugal Renato Sanches, 23. Huenda wakamnunua Sanches kujaza pengo lililoachwa Georginio Wijnaldum, ambaye Liverpool hawana nia ya kumuachilia, japo hawako hawajaridhia ombi la kiungo huyo wa kati wa Uholanzi aliye na umri wa miaka 30, la kutaka mkataba wa miaka minne.

3. Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amepuuzilia mbali tetesi kuwa huenda akarejea Barcelona, huku nyota huyo wa Brazil aliye na umri wa miaka 28- akisisitiza kuwa ameridhika kuwa mjini Paris. 

4. Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amewaomba maafisa wa klabu hiyo kuwasajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Isco, 28, na kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 22, mwezi Januari.

5. Mlinzi wa Chelsea na England Fikayo Tomori, 22, ambaye amehusishwa na Leeds, anajiandaa kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Rennes kwa mkopo hadi mwesho wa msimu. 


EmoticonEmoticon