1. Arsenal na Liverpool
wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves
Bissouma, 24.
2. Tottenham, Everton na Atletico
Madrid wanamuangalia kwa karibu kwa lengo la kumnunua mchezaji wa safu ya
mashambulizi wa Napoli Arkadiusz Milik, 26 raia wa Poland.
3. Barcelona imeanza mazungumzo na
mshambuliaji wa kati Mfaransa France Ousmane Dembele kuhusu mkataba mpya , huku
Manchester United nao wakiendelea kumsaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23
.
4. Manchester United wanapaswa
kumfuta kazi meneja wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer na nafasi yake
ichukuliwe na ama Mauricio Pochettino, Antonio Cone au Diego Simeone, anasema
mmiliki wa wa zamani wa Crystal Palace Simon Jordan.
5. Meneja wa Tottenham Jose Mourinho, 57, anaamini kuwa bado ana miaka ''15 hadi 20 " iliyobaki katika kazi yake ya kufundisha, ikimaanisha kuwa anataka kuwa bado ni meneja wa soka akiwa na miaka 70 na zaidi .
EmoticonEmoticon