Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa December 18, 2020
1. Manchester United huenda
wakawasilisha dau la kumnunua kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 21, japo
mchezaji huyo anadhaniwa kutaka kujiunga na Chelsea endapo ataamua kuondoka
Hammers.
2. Mgombea wa Rais wa Barcelona
Victor Font amesema hatarudia makosa yaliyofanywa na watangulizi wake kutangaza
nia ya kuwanunua wachezaji nyota licha ya kuhusishwa na tetesi za kumnyatia
mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland, 20. Lakini anapanga
kumshawishi Lionel Messi, 33, kusaini mkataba mpya.
3. Wolves inamfuatilia
mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi, 25, ambaye huenda
akaruhusiwa kuondoka mwezi Januari.
4. Arsenal inaonekana inakaribia
kukamilisha usajili wa mchezaji wa safu ya kati na nyuma ya Hertha Berlin Omar
Rekik baada ya mlinzi huyo aliye na umri wa miaka 18-year-kuwasili mjini London
siku ya Alhamisi .
5. Liverpool wamemuongeza mchezaji Roma wa safu ya kati na nyuma Roger Ibanez katika orodha ya walinzi wanaosakwa kujaza pengo lililoachwa na mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Virgil van Dijk, 29, aliyejeruhiwa na huenda wakawasilisha dau la £30m kumnunua Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 22.
EmoticonEmoticon