Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa December 25,
1. Kufutwa kwa kocha wa PSG Thomas
Tuchel kumeathiri matumaini ya klabu ya Real Madrid kumsaini mshambuliaji
Kylian Mbappe kutoka klabu hiyo ya Ligue 1.
2. Beki wa kushoto wa Chelsea
Marcos Alonso pia analengwa na Atletico Madrid, huku mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 29 akikosa fursa ya kukichezea kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya
Stamford Bridge msimu huu.
3. Mkufunzi wa Manchester United
Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsaini beki wa kati mwaka ujao lakini hatajiunga
katika kinyanganyiro cha kumsaini beki wa Austria David Alaba 28, ambaye
kandarasi yake inaisha mwisho wa msimu.
4. Manchester City na Tottenham
zinamchunguza kiungo wa kati wa klabu ya Atalanta na Uholanzi mwenye umri wa
miaka 29 Marten de Roon, ambaye aliwahi kuichezea klabu ya Middlesbrough mapema
akianza kucheza soka.
5. Atletico Madrid inajaribu kumsajili beki wa Arsenal na England mwenye umri wa miaka 23 Ainsley Maitland-Niles kwa mkopo mwezi Januari.
EmoticonEmoticon