Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne December 1, 2020
1. Inter Milan wanataka kumleta
mshambuliaji Mfaransa kutoka Chelsea Olivier Giroud, 34, kwa mkataba wa mkopo
wa miezi sita mwezi Januari, wakiwa na chaguo la kumnunua .
2. Inter Milan pia wanaweza
kukabiliwa na ushindani kutoka mahasimu wa Serie Juventus, kwani meneja Andrea
Pirlo anataka kuwaleta wachezaji wake mwezi Januari, akiwemo Giroud.
3. Liverpool wataweza kusaini
mkataba na mlinzi wa Ajax Perr Schuurs kama watatoa pauni milioni 27 kwa kijana
huyo mwenye umri wa maika 21.
4. Chelsea wataanzisha mazungumzo
na mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, 28, Januari wanataka kumsaini mchezaji
huyo wa Austria kwa mkataba utakaomruhusu kuhama bila malipo wakati mkataba
wake utakapokamilika msimu .
5. Barcelona walikataa dau la euro milioni 250 (£224m) kutoka Inter Milan kwa ajili ya Muargentina Lionel Messi, 33, mwaka 2006, kulingana na rais wa zamani wa klabu hiyo Joan Laporta.
EmoticonEmoticon