Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne Disemba 08

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne December 8, 2020

1. Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema hana shinikizo la kumuuza mlinda mlango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 26, mwenye thamani ya pauni milioni 71.

2. Manchester United inaweza kumgeukia mlinzi wa pembeni wa Real Madrid ya Uhispania, Lucas Vazquez, 29, wakati wanatafuta mshindani wa Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, 23.

3. Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 32, ana uhakika wa 90% wana uhakika atajiunga na Fenerbahce mwezi ujao, kwa mujibu wa mmoja wa wajumbe wa bodi ya Fenerbahce .

4. Wawakilishi wa Jesse Lingard wanapitia ofa za mkopo kwa kiungo huyo wa Manchester United na England mnamo Januari, na Real Sociedad moja ya vilabu ambavyo wamefanya mazungumzo ya awali nae kuhusu mchezaji huyo mwenye miaka 27. 

5. Newcastle wanalenga kurudi katika kambi yao ya Benton Jumanne huku wakitafuta kuendelea na mazoezi baada ya ugonjwa wa Covid-19 kusababisha kuahirishwa kwa mechi yao na Aston Villa. Magpies wanatumai mechi yao na West Brom itafanyika kama ilivyopangwa mwishoni mwa wiki hii. 


EmoticonEmoticon