Tetesi Za Ulaya Jumatano December 2, 2020
1. Manchester United, na Chelsea
zinamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23 mwenye
thamani ya juu.
2. Barcelona wanafuatilia kwa
karibu upatikanaji wa kiungo wa kati -nyuma wa Arsenal Shkodran Mustafi, 28, na
mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, 27, huku wachezaji hao wa kimataifa wa
Ujerumani wakiwa hawatakiwi na klabu zao.
3. Arsenal na Tottenham ni miongoni
mwa klabu kadhaa zenye nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg
Dominik Szoboszlai, 20, huku RB Leipzig, AC Milan na Atletico Madrid pia
wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Hungary.
4. Manchester United, Manchester
City na Chelsea wanashindana kumsaini kiungo wa kati wa Borussia
Monchengladbach na Uswiss Denis Zakaria, 24, mwezi Januari.
5. Tottenham bado wanamtaka mlinzi wa Inter Milan na Slovakia -Milan Skriniar, 25, licha ya mazungumzo kati ya klabu hizo kuvunjika msimu uliopita .
EmoticonEmoticon