Tetesi Za Soka Ulaya
Jumatano December 16
1. Matumaini ya Paris St-Germain
na Manchester City kumsaini Lionel Messi yamefufuliwa upya baada ya mgombea
urais wa Barcelona Emili Rousaud kusema ''ni vigumu kumudu'' mshahara wa
Muargentina huyo baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika msimu ujao. PSG
imeambia maduka yake kujiandaa kwa usajili wa Messi, 33, kutoka Barcelona.
2. Rousaud anataka kuwakutanisha
Messi na mshambuliaji wa Brazil na Paris St-Germain Neymar Uhispania lakini
Barca haina uwezo wa kumudu bei ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 28- kabla ya
mkataba wake kumalizika mwaka 2022.
3. Bayern Munich wako tayari
kumpatia kiungo mshambuliaji wa kati Jamal Musiala, 17, mkataba mpya wa thamani
ya £100,000 kwa wiki licha nyota huyo kunyatiwa na klabu za Ligi Kuu ya England.
4. Wakala wa Mesut Ozil amesema
kiungo huyo wa kati wa Ujerumani aliye na umri wa miaka 32, anataka kusalia
Arsenal kukamilisha miezi sita ya mwisho ya kandarasi yake - Licha ya klabu
hiyo kumtaka aondoke mwezi Januari.
5. West Brom wanajiandaa kumfuta mkufunzi wao Slaven Bilic na kumpatia nafasi yake kocha wa zamani wa England Sam Allardyce.
EmoticonEmoticon