Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu December 21, 2020
1. Real Madrid ina matumaini ya
kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka klabu ya Paris
St-Germain msimu ujao.
2. Liverpool inafikiria kumuuza
mshambuliaji wa Misri asiye na raha Mohamed Salah, 28, kulingana na
mshambuliaji wa zamani wa Misri Mohamed Aboutrika.
3. Mwenyekiti wa klabu ya Bayern
Munich Karl-Heinz Rummenigge amekubali kwamba beki David Alaba, 28, anatarajiwa
kuondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani.
4. Manchester United ina hamu ya
kumsajili mchezaji anayelengwa na Arsenal pamoja na liverpool Yves Bissouma,
mchezaji wa klabu ya Brighton na raia wa Malian mwenye umri wa miaka 24 ambaye
ameonesha mchezo mzuri msimu huu.
5. Mkufunzi wa Juventus Andrea Pirlo amepinga uwezekano wa uhamisho wa nyota wa Argentina Paulo Dybala, 27.
EmoticonEmoticon