Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano Disemba 23

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano December 23, 2020

1. Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa klabu kadhaa ambazo tayari zimekwisha eleza nia yao ya kumchukua mlinzi wa klabu ya Schalke Ozan Kabak, 20, huku klabu hiyo ya Bundesliga c ikishusha bei yake na sasa ikitaka ilipwe pauni milioni 25 badala ya milioni 40 kwa ajili ya mchezaqji huyo wa kimataifa wa Uturuki.

2. Liverpool wana uhakika wa kupata ofa kutoka kwa mshambuliaji wao kutoka Misri Mohamed Salah, 28, na kumuongezea malipo yake ya pauni 200,00-kila wiki ili kuzima nia ya Real Madrid, Barcelona na Paris St-Germain ya kumchukua .

3. Liverpool wamejiunga na Manchester United na Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaini Jack Grealish, 25, huku Aston Villa wakitaka dau kwa ajili ya kiungo wao wa kati wa England. 

4. Mgombea wa wadhifa wa rais wa Barcelona Jordi Farre anasema klabu hiyo inahitaji kuimarisha safu yake ya mashambulizi na akamtaja mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 23, miongoni mwa wachezaji anaowahusudu.

5. Jordi Farre mwenye umri wa miaka 45-pia ameahidi kumsaini tena Neymar kutoa pizza za bure na tattoos kwa klabu. Wachezaji wa Arsenal wanakapiliwa na punguzo la 25% la ushuru iwapo watashuka daraja kutoka Primia Ligi. Punguzo hilo la mshahara wao litafiukia pauni milioni 37.5 ambazo zitakatwa kwenye mishahara yao.


EmoticonEmoticon