Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu Disemba 28

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu December 28, 2020

1. Arsenal wamempeana mchezaji nyota wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, kwa Juventus kwa mkopo wa miezi sita na wako tayari kupunguza marupurupu yake kuhakikisha ofa hiyo inafanikishwa.

2. Manchester United wamejiondoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, ambaye huenda akapatikana kwa uhamisho wa bure msimu ujao. Klabu hiyo ya The Old Trafford inahoji bei ya kiongo huyo raia wa Austria aliye na umri wa miaka 28 ambaye anacheza safu ya kushoto na nyuma.

3. Arsenal wana matumaini ya kuzipiku Manchester City na Bayern Munich katika mbio za kupata saini ya Tariq Lamptey, 20, kutoka Brighton, ikiwa iHector Bellerin, 25, ataamua kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Barcelona.

4. Juventus wanafikiria uhamisho wa Januari ili kumnasa kiungo wa zamani Paul Pogba kurudi Turin, lakini watahitaji Manchester United kukubali dauni la pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa miaka 27.

5. Paris St-Germain iko tayari kuipatia Inter Milan kiungo wake wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 26 Leandro Paredes ili kubadilishana na kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 28.


EmoticonEmoticon