Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi Disemba 03

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi December 3, 2020

1. Meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino yuko mbele ya kocha wa kikosi cha akiba cha Real Madrid Raul kama mgombea anayeongoza miongoni mwa wagombea wanaowania kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane, iwapo Real wataamua kumfuta kazi Mfaransa huyo.

2. Inter Milan watajiandaa kumuuza mlinzi Mslovakia Milan Skriniar, 25, kwa Tottenham kwa pauni milioni 45 mwezi ujao. 

3. Pochettino anadhaniwa kuwa yuko makini kuhamia Paris St-Germain na anaweza kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel. 

4. Zidane amepoteza imani na wachezaji wake kadhaa ikiwa ni pamoja na winga wa zamani wa Chelsea Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 29- ambaye ni mchezaji wa kimataifa kutoka Ubelgiji.

5. Meneja wa Tottenham Jose Mourinho anasema ni jukumu lake kuamua iwapo klabu hiyo itamuuza kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, mwezi Januari au la.


EmoticonEmoticon