Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano Disemba 30

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano December 30, 2020

1. Manchester City inasalia na matumaini kwamba itamsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi 33, mwaka 2021, licha ya nahodha huyo wa Barca kusema kwamba anatumai kwamba siku moja atacheza soka nchini Marekani. 

2. Arsenal wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid Isco, 28, wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa. The Gunners, ambao wanataka kumsaini mchezaji huyo kwa mkopo wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa sevilla.

3. Mauricio Pochettino anatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji wa Tottenham ikiwemo kiungo mshambuliaji Dele Alli, 24, na kipa wa Ufaransa Hugo Lloris, iwapo kocha huyo raia wa Argentina atathibitishwa kuwa mkufunzi Paris-St Germain.

4. Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ataamua wiki hii iwapo atatia saini kandarasi mpya na klabu ya Liverpool huku kocha wa Barcelona Ronald Koeman akiwa na matumaini ya kumshawishi kiungo huyo kujiunga na Barcelona.

5. Kandarasi ya Wijnaldum, ambaye amekuwa Anfield tangu 2016 inakamilika mwezi Juni. Liverpool imesitisha hamu ya kumsajili beki wa kati wa Inter Milan Milan Skriniar, 25, baada ya kukasirishwa na dau la £54m lililowasilishwa na klabu hiyo ya Itali.


EmoticonEmoticon