Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu Disemba 07

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu December 7, 2020

1. Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 27, amepata ofa za timu kubwa sita za ligi ya Primia-Manchester United, Liverpool, Chelsea, Tottenham, Manchester City na Arsenal. 

2. Wadhamini wa shati wa Manchester United Chevrolet wanaamini itakuwa jambo la thamani kibiashara kusaidia kufadhili hatua ya kumrejesha, Old Trafford mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 35.

3. Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 32, anaamini kuwa ataweza kupata klabu nyingine bora - lakini ana uwezekano wa kuondoka kabla ya msimu ujao.

4. Kiungo wa kati wa Liverpool, Mholanzi Georgio Wijnaldum, 30, amedokeza kuwa anasubiri klabu ichukue hatua kuhusu kuongeza mkataba wake.

5. Manchester United inamfuatilia mlinzi wa Kiingereza wa Atletico Madrid Kieran Trippier, 30, huku Ole Gunnar Solskjaer akimuhitaji pia kwa ajili ya kumpa changamoto Aaron Wan-Bissaka, 23.


EmoticonEmoticon