Maofisa
nchini India wanachunguza ugonjwa ambao haujafahamika uliosababisha zaidi ya
watu 140 kulazwa mwishoni mwa wiki hii.
Wagonjwa hao kutoka mji wa Eluru huko Andhra Pradesh,
wamekuwa na dalili za kichefuchefu na kukosa nguvu, daktari ameeleza.
Hospitali ya serikali ya Eluru imetenga vitanda kadhaa kwa
ajili ya wagonjwa wa ugonjwa huo usiojulikana kama vitahitajika.
Ugonjwa huo unakuja wakati India ikiwa inakabiliwa na mlipuko
wa janga la corona.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa wagonjwa hao walifanyiwa
vipimo vya corona na wote wakawa hawana virusi vya corona.
Maafisa wa afya wa hospitali ya Eluru wameiambia 'The Indian
Express': "Watu wa India wanaugua, haswa watoto , ghafla tu wanaanza
kutapita baada ya kulalamika kuwa macho yao yanawasha.
Wengine wanazimia au kukosa nguvu kabisa.
Wengi wao waliopelekwa hospitali wanaonekana kupona kwa
haraka na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Waziri wa afya wa Andhra Pradesh Alla Kali Krishna Srinivas
alisema sampuli za damu zao hazikuona ushaidi wowote wa maambukizi yatokanayo
na virusi.
"Tunachunguza maji na hewa katika eneo ambalo watu
wanaugua ugonjwa huo," alisema. "Ugonjwa huu wa ajabu utadhibitika tu
mara baada ya matokeo ya maabara yatakapotoka."
Hata hivyo wanasiasa wa upinzani kutoka chama cha Telugu Desam ,wametaka ufafanuzi wa sababu ya kuibuka kwa ugonjwa huo wa ajabu.
Credit : Bbc
EmoticonEmoticon