Bunge la
Iran limepitisha sheria ya kuwazuia wachunguzi wa Umoja wa Mataifa katika
maeneo yao ya shughuli za kinyuklia na kuongeza uzalishaji wake wa Urani.
Sheria hiyo itaitaka serikali kurejelea urutubishaji wa urani
kwa asilimia ishirini.
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema anapinga kupitishwa kwa
sheria hiyo ambayo inakiuka makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kati ya Iran na
nchi zenye nguvu zaidi ulimwenguni ya kudhibiti mpango wa kinyuklia wa nchi
hiyo kutokwenda zaidi ya asilimia 3.67 na kuongeza itahujumu diplomasia.
Bunge la Iran linataka wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wa
kudhibiti silaha za kinyuklia kuzuiwa kuchunguza vitu vya kinyuklia na kuongeza
uwezo wake wa kuzalisha urani katika kinu cha Natanz na Fordow iwapo vikwazo vya
kiuchumi dhidi ya Iran havitaondolewa katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
Vikwazo hivyo vilivyolenga sekta ya mafuta na fedha ya Iran vilirejeshwa na nchi za magharibi baada ya Marekani kujiondoa kutoka makubaliano hayo ya kihistoria yaliyofikiwa 2015.
EmoticonEmoticon