Irani Yafanya Maziko Ya Mwanasayansi Wao Wa Nyukila

 

Iran imefanya ibada ya maziko ya aliyekuwa mwanasayansi Mohsen Fakhrizadeh aliyeanzisha program ya nyuklia ya taifa hilo miongo miwili iliyopita. Waziri wa ulinzi aapa kuiendeleza kazi ya mwanasanyansi huyo. 

Jeshi maalumu la heshima, leo lilibeba jeneza la mwili wa mwanasayansi Mohsen Fakhrizadeh aliyeripotiwa kuuawa kwa mbinu ya kijeshi ya kushtukiza Ijumaa iliyopita. Maafisa wa Iran wanaituhumu Iran kuwa ndiyo iliyohusika na shambulio hilo. 

Mwanasayansi huyo aliyeuawa alikuwa mkuu wa program ya AMAD, ambayo Israeli na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakiituhumu kuwa ni operesheni ya kijeshi inayofanya upembuzi yakinifu ili kutengeneza silaha za nyuklia.

Miongoni mwa waliohudhuria ibada ya maziko ya Mohsen Fakhrizadeh ni pamoja na waziri wa ulinzi, Amir Hatami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran Jenerali Hossein Salami, mkuu wa mpango wa nyuklia wa kiraia Ali Akbar Sahei waziri wa Intelijensia  Mamoud Alavi. 

Katika shughuli hiyo waziri wa ulinzi wa Iran Amir Hatami alizikosoa nchi ambazo hadi sasa hazijalaani mauaji ya Fakhrizadeh huku waziri wa ulinzi akiapa kuwa Iran italipiza kisasi kwa mauaji hayo. 

"Na maadui wanapaswa kufahamu kuwa, wameshindwa kwa mara ya kwanza. Kama walidhamiria kumuua shujaa wetu ili jina lake lipotee, sasa jina lake linaimwa kila mahali na amekuwa mfano kwa wote wanaoianza safari ya mapambano.


EmoticonEmoticon