Jeshi la
Ethiopia limewaua zaidi ya watu 40 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya zaidi ya
watu 100 ikiwemo watoto katika eneo la Benishangul-Gumuz , vyombo vya habari
vimesema.
Maafisa watano wa serikali ya sasa na wenzao wa zamani pia
walikamatwa kufuatia tatizo hilo la kiusalama , ripoti zimeongeza.
Washukiwa hao walichoma nyumba za wanavijiji waliokuwa
wamelala kuwapiga risasi na kuwachoma visu wakati wa shambulio hilo la siku ya
Jumatano.
Shambulio hilo linajiri siku moja baada ya waziri mkuu Abiy
Ahmed kuzuru eneo hilo. Haijulikani washambuliaji ni akina nani lakini
walionekana kulenga jamii za makabila madogo yaliowasili na kuishi katika eneo
hilo , kulingana na Amnesty International.
Ethiopia imeshuhudia ongezeko la ghasia za kisiasa, kikabila na kidini katika miaka ya hivi karibuni.
EmoticonEmoticon