Joe Biden Asema Utawala Wa Trump Umeharibu Vitengo Vya Usalama

 

Vitengo muhimu vya usalama vimefanyiwa uharibifu mkubwa chini ya utawala wa rais Donald Trump , rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema.

Bwana Biden alisema kwamba timu yake haipati habari inazohitaji kutoka kwa idara ya ulinzi wakati ambapo inajiandaa kuchukua mamlaka.

Alizungumza baada ya kupatiwa habari na maafisa wa usalama pamoja na wale wa masuala ya sera za kigeni.

Katika hotuba alioitoa katika mkutano wa video bwana Biden alisema kwamba kundi lake linakabiliwa na vizuizi katika idara ya ulinzi hususan afisi ya usimamizi na bajeti.

''Kufikia sasa , hatupati habari zote ambazo tumehitaji kutoka kwa utawala unaoondoka katika vitengo muhimu vya usalama'', alisema. ''Kwa upande wangu huo ni ukosefu wa uwajibikaji''.

Rais huyo mteule aliongezea kwamba kundi lake lilitaka kujua hali ya wanajeshi wa Marekani kote duniani na kwamba maadui wa taifa hilo huenda wakachukulia tofauti zilizopo na kusababisha mkanganyiko. 

Alisema kwamba idara nyingi muhimu za kiusalama zimefanyiwa uharibifu mkubwa. Nyingi hazina maafisa wa kutosha na motisha iko chini. Sera zilizokuwa zikitumika hazina tena thamani ama hata zimetupiliwa mbali.


EmoticonEmoticon