Rais mteule
wa Marekani Joe Biden ameteua maafisa wa ngazi ya juu kusimamia uchumi wa
Marekani unaoathiriwa na janga la virusi vya Corona.
Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Benki
Kuu ya Marekani Janet Yellen, ambaye anakuwa mwanake wa kwanza kuwa waziri wa
fedha katika historia ya miaka 231 ya wizara hiyo.
Biden amemteua Neera Tanden, kuwa mkuu wa ofisi ya kusimamia
utawala na bajeti ya serikali. Iwapo ataidhinishwa na senate, Tanden atakuwa
mwanamke wa kwanza, Mmarekani mwenye asili ya Afrika kuongoza Idara hiyo.
Wally Adeyemo, ameteuliwa kuwa naibu wa waziri wa fedha,
akiwa mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuteuuliwa katika nafasi hiyo.
Wengine walioteuliwa ni Pamoja na mchumi Cecilia Rouse, kuwa
mkuu wa baraza la washauri wa uchumi katika white house.
Anakuwa mwanamke wa kwanza, mmarekani mwenye asili ya Afrika
kushikilia nafasi hiyo.
Janga la Corona limeathiri sana uchumi wa Marekani ambao ndio
mkubwa zaidi duniani.
Wanawake wameteuliwa kuongoza timu nzima ya mawasiliano white house.
EmoticonEmoticon