Joe Biden Azungumza Baada Ya Kuidhinishwa Rasmi

Joe Biden amesema kuwa "utashi wa watu umeshinda " baada ya ushindi wake wa uchaguzi kuthibitishwa na wajumbe wa uchaguzi wa Marekani - US electoral college.

Katika hotuba aliyoitoa baada ya kutangazwa kwa ushindi huo , alisema kuwa demokrasia ya Marekani ''imesukumwa na kujaribiwa '' na "imedhihirisha kuwa ni jasiri, ya kweli na thabiti ''.

Bw Biden pia amezungumzia kuhusu hatua ya Trump ya kujaribu kupinga matokeo ya uchaguzi.

Kuthibitishwa kwa ushindi huo ni mojawapo ya hatua alizohitaji Bw. Biden ili kumuwezesha kuchukua mamlaka ya urais.

Rais Trump bado hajatoa kauli yoyote. Muda mupi baada ya matokeo kuthibitishwa, alitangaza kwenye ukurasa wa Twitter kuondoka madrakani kwa Mwanasheria Mkuu William Barr, ambaye alisema kuwa hapakuwa na wizi ushahidi wa wizi wa kura katika uchaguzi, licha ya madai ya rais.

Akizungumza katika jimbo la Delaware, Bw Biden alisifu wale aliowaita "wanaume na wanawake wa kawaida " ambao walikataa kunyanyaswa, akizungumzia juhudi za rais za kuhoji na kubadilisha matokeo ya uchaguzi , akihusisha mashitaka ya kisheria ambayo yamekuwa yakikataliwa na mahakama kote nchini Marekani.

"Moto wa demokrasia uliwaka zamani katika nchi hii ," alisema . "Na tunafahamu kwamba hakuna lolote hata janga la ugonjwa au ukiukaji wa mamlaka unaweza kuzima mioto hiyo ."

Bw Biden alisema kuwa ni muda wa "kugeuza ukurasa, kama ambavyo tumekuwa tukifanya katika kipindi chote cha historia -kuungana na kupona". 


EmoticonEmoticon