Johnson Kwenda Brussels Kwa Mazungumzo Zaidi Ya Brexit

 

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kwenda Brussels kwa ajili ya majadiliano ya kina baada ya mazungumzo ya muda mrefu ya simu na rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen. Hata hivyo wakuu hao wawili wanakiri kwamba bado kuna tofauti baina yao. 

Taarifa ya pamoja kutoka kwa waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen hapo jana Jumatatu imesema kwamba masharti ya makubaliano bado hayajafikiwa.

Taarifa hiyo imesema walikubaliana kwamba masharti ya kukamilisha makubaliano hayakuwepo kwa sababu ya tofauti kubwa iliyobaki juu ya maswala matatu muhimu ya mazingira ya usawa kwenye ushindani wa kibiashara, makubaliano ya masuala ya uvuvi na usimamizi na uendeshaji wa mambo hayo.

Taarifa hiyo ilisema wamewaomba wawakilishi kwenye mazungumzo hayo kuandaa muhtasari kuhusiana na tofauti hizo zilizosalia na zinazotakiwa kujadiliwa kwenye mkutano utakaowakutanisha ana kwa ana mjini Brussels katika siku zijazo.


EmoticonEmoticon