Kampuni ya
kutengeneza dawa ya Moderna imesema kwamba inataka idhini ya dharura kwa ajili
ya kutumia chanjo yake dhidi ya virusi vya Corona hapa nchini Marekani na
Ulaya.
Hii ni baada ya chanjo hiyo kuonyesha ufanisi wa asilimia 94.
Ombi hilo lina maana kwamba maafisa wa afya wanaweza kutumia
chanjo hiyo kuanzia katikati mwa mwezi Desemba.
Kampuni ya Moderna imesema kwamba imekamilisha kufanyia
majaribio chanjo hiyo, kati ya watu 30,000 na matokeo yake yalikuwa mazuri
sana.
Hatua ya kampuni za Modern ana Pfizer kuomba kuanza kutumia
chanjo yake kwa matumizi ya dharura, inajiri wakati idadi ya watu
wanaoambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani ikiwa inaongezeka kwa kasi
sana.
Maelfu ya watu wanagunduliwa kuambukizwa virusi vya Corona
nchini Marekani kila siku.
Maafisa wa afya wameeleza wasiwasi kwamba idadi ya maambukizi huenda ikaongezeka zaidi kwa sababu watu wamekataa kuzingatia maagizo ya afya kuzuia maambukizi.
EmoticonEmoticon