Argentina inakuwa
moja kati ya nchi chache za Amerika Kusini kuruhusu utoaji mimba baada baraza
la Senati la Bunge la nchi hiyo kuidhinsha usiku wa Jumanne sheria ya
kihistoria iliyopingwa vikali na Kanisa Katoliki.
Waungaji mkono wa sheria hiyo wakivaa nguo za kijani wamekuwa
wakisherekea mjini Buenos Aires tangu jana usiku.
Baadhi ya waliojitokeza kusheherekea kupitishwa kwa sheria
hiyo walionekana wakitokwa na machozi.
Rais wa Seneti Cristina Kirchner alithibitisha uamuzi huo
baada ya zaidi ya saa 12 za majadiliano.
Maelfu ya wanawake hutoa mimba kila mwaka katika taifa hilo
ambapo karibu watu 3,000 hufariki kwa kutumia njia za kienyeji na haramu
amesema rais Alberto Fernandez aliyependekeza mswada huo mapema mwaka huu.
Hii ina maana utoaji mimba unaruhusiwa katika taifa anakotoka
Papa Francis hadi wiki ya 14 ya ujauzito.
Hadi hivi sasa ni Uruguay, Cuba na Guyana ndio ambazo zinazoruhusu utoaji mimba kwa hiyari huko Kusini mwa Amerika.
EmoticonEmoticon