Katibu Mkuu
Umoja wa Mataifa, Antonio
Guterres ametoa
wito kuwa kusiwepo na upendeleo katika ugawaji wa chanjo ya virusi vya corona
na kwamba kila nchi ina haki ya kupata chanjo hiyo zikiwemo nchi za Afrika.
Akizungumza
kwa njia ya video kwenye mkutano na Umoja wa Afrika, Guterres amesema anaona
utaifa ukipewa kipaumbele kwenye suala la chanjo huku nchi tajiri zikipewa
nafasi kubwa kuliko maskini.
“Bidhaa ya
umma inapatikana kwa watu wote, kila mahali duniani na hasa barani Afrika
ambako kuna mahitaji makubwa ya kukabiliana ipasavyo na msukosuko huo” Guteres
Hivi karibuni shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, lilifichua kuwa nchi tajiri duniani zimenunua chanjo mara tatu zaidi ya zinavyohitajika, jambo ambalo linaweza kuwakosesha chanjo mabilioni ya watu katika nchi masikini.
EmoticonEmoticon