Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ataka Chanjo Ya COVID-19 Ipatikane Kwa Wote

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza ulazima kwa chanjo ya virusi vya corona kupatikana kote duniani katika wakati mataifa tajiri yanazindua kampeni ya kutoa chanjo kwa raia wake. 

Katika hotuba yake mbele ya Bunge la Ujerumani, Bundestag, Guterres amesema ni muhimu kwa nchi tajiri kusaidia ununuaji wa chanjo ya COVID-19 kwa nchi masikini na kuepuka kujilimbikizia shehena ya dozi. 

Guterres pia amewasifu watafiti wa kampuni ya Ujerumani ya BioNTech kwa kushirikiana na kampuni ya Marekani ya Pfizer na kuwashinda wapinzani wao kwenye mchuano wa kutafuta chanjo ya COVID-19. 

Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Kansela Angela Merkel akisema uongozi wake madhubuti na uliojaa busara umeisaidia Ujerumani kwenye kipindi chote cha janga la virusi vya corona.


EmoticonEmoticon