Katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema viongozi wa dunia wanapaswa kutangaza ''dharura ya hali ya hewa'' kwenye nchi zao ili kuchochea hatua za kuepusha janga la ongezeko la joto duniani. 

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiufungua mkutano wa kilele kuhusu hali ya hewa unaofanyika mjini London, Uingereza kwa njia ya video. Katika mkutano huo, viongozi wa ulimwengu wanatarajiwa kutangaza mipango zaidi ya kupambana na ongezeko la joto duniani. 

Hayo yanajiri ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu ya miaka mitano tangu kutiwa saini mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa wa kihistoria huko mjini Paris mnamo mwaka 2015. 

Kwa upande wao viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya jana walithibitisha lengo la kupunguza uzalishaji wa hewa ya kaboni kwa asilimia 55 ifikapo mwaka 2030.


EmoticonEmoticon