Katika harakati za kupambana na
Ugonjwa wa corona, Kenya imeagiza dozi Milioni 24 za Chanjo ya Corona Virus
zitakazotosha 20% ya Wakenya.
Dozi hizo zinagharimu Ksh.
Bilioni 10 sawa na takriban Tsh. Bilioni 207.83, kiasi ambacho kitachangiwa na
Mataifa yaliyoendelea hivyo kila dozi itagharimu Ksh. 320 sawa na Tsh. 6,600.
Katibu Mkuu wa Afya, Patrick
Amoth amesema Wafanyakazi waliokuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi pamoja
na Wazee watapatiwa Chanjo hiyo.
Kenya inakuwa nchi iliyoagiza dozi nyingi zaidi kwa nchi za Afrika Mashariki, Uganda iliagiza dozi Milioni 9.
EmoticonEmoticon