Kiongozi wa
jimbo la kaskazini la Ethiopia linaloshuhudia mapigano la Tigray Debretsion
Gebremichael amemwambia Waziri Mkuu Abiy Ahmed aache ukorofi na aondoe
wanajeshi wake mara moja.
Amemtaka Abiy kuondoa wanajeshi hao katika jimbo hilo ambalo
Gebremichael anadai linaendelea kushuhudia mapigano makali licha ya serikali
kutangaza ushindi siku mbili zilizopita.
Kupitia mahojiano kwa njia ya simu na shirika la habari la
Reuters mapema Jumatatu, kiongozi huyo wa chama cha Tigray People’s Liberation
Army, TPLF, amesema kuwa bado yuko kwenye mji mkuu wa jimbo hilo wa Mekelle,
licha ya serikali kudai kuuteka Jumamosi.
Ameongeza kusema kuwa kinyume na madai ya Abiy kuwa
wameshinda, mapigano yanaendelea na kwamba ushindi utakuwa wao.
Gebremichael amesema pia baadhi ya wanajeshi wa Eritrea
wanaosaidiana na wanajeshi wa serikali wameshikiliwa na wapiganaji wake.
Wakati huo huo, Abiy amekiambia kikao maalum cha Bunge la Ethiopia mapema leo kuwa hakuna raia hata mmoja alieuwawa kwenye mashambulio hayo yaliyoanza Novemba 4 dhidi ya vikosi vya TPLF.
EmoticonEmoticon