Kura Moja Yavunja Serikali Kosovo

 

Huko Kosovo, Serikali ya Avdullah Hoti iliyoundwa mwezi Juni nchini humo, imevunjwa  baada ya kupoteza kura ya imani iliyopigwa bungeni. Kufuatia hali hiyo, uchaguzi utarudiwa tena nchini humo.

Kura ya moja ya Mbunge ambayo haikuhesabiwa kutokana na hukumu yake ya kifungo cha miezi 15 gerezani, ilisababisha kukosa kura ya imani kwa ajili ya kuunda serikali.

Kwa uamuzi huo wa Mahakama ya Katiba, Serikali iliyokuwa imeundwa mwezi Juni kwa ushindi wa tofauti moja ya kura katika kura ya imani bungeni, ililazimika kuvunjwa.

Uchaguzi unatarajiwa kuandaliwa tena nchini humo ndani ya siku 40.

Kufuatia kujiuzulu kwa Rais wa zamani wa Kosovo, Hashim Thaji, Novemba 5, Spika wa Bunge, Vjosa Osmani amekabidhiwa jukumu la kuhudumu kama Rais.

Osmani atakutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini kuamua tarehe ya uchaguzi.


EmoticonEmoticon