Kwa Miaka 26 Ameficha Jinsia Ambayo Sio Ya Kike Wala Ya Kiume Mtanzania

 

Baby John Musamba mwenye umri wa miaka 26 alizaliwa katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Lakini badala furaha ya wazazi wake kujaliwa mwana iligeuka mshangao. Mtoto wao alikuwa na maumbile ya ajabu. 

Musamba alizaliwa bila sehemu za siri za mtoto wa kiume au kike. Alianza kufahamu hali yake pindi alipotimiza miaka mitano hivi alipogundua kwamba alikuwa tofauti na watoto wengine.

Wakati huo wazazi wake walimpa nasaha ya kujikubali alivyo. Anasema kuwa jamaa zake wa karibu walisimama naye na kuhakikisha kuwa wamelinda kile kilichokuwa siri ya maumbile yake. Baby aliandikishwa kama mtoto wa kike alipozaliwa, na hata kwenye vitambulisho vyake vya kuzaliwa vimenakili hivyo.

Alipozaliwa wazazi wake walihesabu watoto wao kama mabinti wawili na kaka watatu. Hata hivyo, kwa ndani familia hiyo ilihesabiwa kuwa na binti mmoja na kaka watatu na yeye ambaye ana jinsia yenye utata.

Musamba anasema kwa maumbile yake ya ndani, hana viungo vya uzazi vya kiume wala vya kike. Ana sehemu ndogo tu ya kwenda haja ndogo.

Kati ya sehemu hiyo na sehemu ya kwenda haja kubwa ni mfupa tu. Pia anasema kuwa hana matiti ila, muonekano wake una umbo la kike .

Baby amefanyiwa uchunguzi mara nyingi maishani, akiwa na miaka miwili, akiwa na miaka sita, kumi na 20. Nyakati zote, uchunguzi umebaini kuwa hana viungo vyovyote vya kuashiria kama yeye ni wa kike au kiume.

Full Story:Bbc


EmoticonEmoticon