Maelfu ya
waandamanaji Jumanne wamekusanyika kwenye mji mkuu wa Armenia wa Yerevan,
wakiongozwa na upinzani kwenye kampeni ya kushinikiza waziri mkuu Nikol
Pashinyan, ajiuzulu kutokana na mkataba wa mwezi Novemba na Azerbaijan ikilenga
kusitisha mapigano.
Waandamanaji hao waliokuwa kwenye bustani kuu mjini humo
walisikika wakisema kuwa Nikol ni msaliti wakati maafisa wa usalama wakishika
doria kwenye ofisi za kiongozi huyo zilizoko karibu.
Kundi lingine linasemekana kuingia kwenye majengo ya serikali na kuzua vurugu huku wengine wakisemekena kufunga barabara kuu.
Kiongozi wa
muungano wa upinzani wenye vyama zaidi ya darzeni moja ameapa kuitisha
maandamano ya kila siku hadi pale Pashinyan atakapo kubali kukabidhi madaraka
kwa serikali ya mpito itakayo twikwa jukumu la kuitisha uchaguzi wa bunge ndani
ya kipindi cha mwaka mmoja.
Vazgen Manukian ambaye ameidhinishwa na muungano huo kwa jina National Salvation Movement, kuongoza serikali ya mpito ameomba jeshi la Armenia pamoja na polisi kukaidi amri za Pashinyan na kujiunga na watu wengine. Awali Pashinyan aliweka wazi kuwa hakuwa na nia ya kuondoka madarakani.
EmoticonEmoticon