Mahakama
moja nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanamke mwanaharakati wa haki za
binadamu Loujain al-Hathloul kutumikia kifungo cha karibu miaka sita.
Chombo cha habari cha Sabq chenye uhusiano na serikali
kimesema mahakama ya kupambana na ugaidi ya Saudi Arabia imemkuta al-Hathloul
na hatia ya uchochezi wa kuleta mabadiliko, akifuata ajenda ya kigeni na kutumia
mtandao wa intaneti kuharibu utulivu wa umma.
Al-Hathloul amekuwa jela tangu mwaka 2018 baada ya kukamatwa
pamoja na wanawake wengine raia wa Saudi Arabia wasiopungua darzeni moja ambao
ni wanaharakati wa haki za binadamu.
Alikuwa anataka kuwepo mageuzi kama vile sheria ya mwanaume
kumsimamia mwanamke na kuwaruhusu wanawake haki yao ya kuendesha magari.
Kesi ya mwanamke huyu imekosolewa na wataalam wa haki za binadamu wa UN, makundi ya haki za binadamu na wabunge wa Marekani na Umoja wa Ulaya.
EmoticonEmoticon