Mahakama Ufaransa Imewakuta Na Hatia Watu 14 Kwa Kuhusishwa Na Shambulizi La Ugaidi

 

Mahakama nchini Ufaransa umewahukumu watu 14 hukumu ya kifungo cha kati ya miaka 4 hadi maisha gerezani kwa kuhusishwa na shambulizi la kigaidi la 2015 la jarida la tashtiti la Charle Hebdo. 

Miongioni mwa 14 hao yupo alietajwa kuwa mshtikiwa mkuu  Ali Riza Polat, ambaye amekutwa na makosa kuyapanga mashambulizi hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani, Kijana wa umri wa miaka 35, mwenye asili ya Kifaransa na Kituruki amekutwa na hatia ya kusaidia na kuchochea uhalifu wenye dhamira ya kigaidi ikiwa na miongoni na mashitaka mengine pia amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.

Polat, ambae mara zote amekuwa akikanusha tuhuma hizo alisikika wakati wa hukumu akisema kwa sauti kwamba hicho kilichosemwa ni uongo. 

Lakini wote hao walikuwa katika mashtaka hayo walihusishwa kwa kutoa misaada kwa wahalifu kwa kuwapa misaada au vifaa kama gari. 

Aidha katika hukumu hiyo pia, mahakama iliweza kuyatupilia mbali mashtaka kadhaa ambayo dhidi ya watumiwa ambayo yaliwasilishwa na waendesha mashtaka.


EmoticonEmoticon