Malawi Yatangaza Hatua Kali Dhidi Ya Wanyanyasaji Kijinsia

 

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza mipango ya adhabu kali dhidi ya wale wanaofanya unyanyasaji wa kijinsia, baada ya kuongezeka kwa kesi na aina hiyo wakati wa janga la corona. 

Katika hotuba yake ya kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Desemba 10, Chakwera alisema Malawi pia itahitaji kufundishwa kwa haki za binadamu mashuleni.

Rais Chakwera alisema takwimu inayoonyeshwa na idara ya taifa ya takwimu za ghasia za kijinsia inaogopesha.

“Miaka mitatu iliyopita, Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu iliripoti kwamba mmoja kati ya wanawake na wasichana watatu wa Malawi kati ya miaka 15 hadi 49 anapata unyanyasaji wa kingono au kimwili. 

Na kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, kesi za uhalifu huu zimekuwa zikiongezeka. Na katika miezi mitatu iliyopita ya mwaka huu pekee, kiwango kimekuwa juu kwa asilimia 35 kuliko kipindi hicho hicho mwaka jana.” Aliongeza Chakwera.

Chakwera alisema mwelekeo huo unaonyesha kuwa chini ya vizuizi vya kutoka vilivyowekwa ili kupambana na COVID-19, uhalifu wa kijinsia umeenea. Alitangaza mipango ya adhabu kali dhidi ya wale wanaofanya vurugu za kijinsia.

“Wizara za Sheria, Jinsia na utawala zitaandaa marekebisho ya sheria husika ikiwa ni pamoja na Utaratibu wa Makosa ya Jinai na nambari ya Ushahidi ili kuharakisha kushughulikiwa kwa kesi kama hizo, kutoa adhabu kali za lazima dhidi ya wakosaji na kuanzisha sajili ya wahalifu wa kijinsia.”alisema Chakwera.


EmoticonEmoticon